Na James Timber, Mwanza
Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe, inayojihusisha na utetezi wa watu wenye ulemavu wa ngozi yenye Makao yake Makuu nchini Uholanzi, inatarajia kuongoza mataifa zaidi ya  18 kupanda mlima Kilimanjaro, lengo likiwa ni kuvunja ukimya juu ya matukio ya Ukatili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.

Akiongea na Vyombo vya Habari jijini hapa Mkurungenzi wa Taasisi hiyo Josephat Torner amesema zoezi hilo litaanza Septemba  21, mpaka Septemba 28, Mwaka na kila mgeni atakayepanda Mlima Kilimanjaro atalipa kiasi cha Dola elfu moja na pesa hiyo itaenda katika mfuko wa elimu na itatumika kusambaza elimu kuwafikia watu wengi zaidi ikiwa ni pamoja na kuiongezea serikali kipato.

"Jambo ambalo linakeuka haki zetu za msingi ni  kumzika mtu mwenye ulemavu wa ngozi ndani ya nyumba kwa kuwaogopa watu wanaofukua viungo kwa lengo kujipatia utajiri, jambo ambalo halina uhalisia," alisema Torner.

Amesema mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi umepungua lakini wamekuja na njia nyingine ya utoji kucha na kuwang'oa nywele kisha kwenda kuuza na kufanyia matambiko.

Pia ameiomba Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dk.John Magufuli kupitia vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanaongeza ulinzi katika mipaka kwani wanaamini uhamiaji haramu unachangia ongezeko wa matukio hayo.

Aidha baadhi ya nchi zitakazoshiriki kujumuika pamoja katika kupanda Mlima Kilimanjaro ni Malawi, Kenya, Uganda Kongo, Senegal, Uholanzi, Japan, Australia, Amerika, Italia, Sweeden na Uingereza.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: