Saturday, 14 April 2018

Mambo matano usioyajua baada ya Alikiba Kuoa

Kama tulivyokuhabarisha hapo jana kuwa msanii wa muziki Bongo, Alikiba anaona huko Mombasa nchini Kenya, ni kweli hilo limejiri licha ya kugubikwa na usiri mkubwa.
Alikiba amemuoa mrembo Aminah Rekish ambaye inaelezwa kuwa anafanya kazi ya Fiscal analyst (Mchambuzi wa masuala ya fedha) serikalini, kaunti ya Mombasa.

Mwandishi wa habari kutoka Nairobi Kenya, Changez Ndzai amedai mara baada ya shughuli ya hapo jana leo hii pia kuna tarajiwa kuwa na hafla fupi ambayo Gavana wa Mombasa, Hassan Ali Joho anatajiwa kuwepo.
Ameeleza pia hafla ya leo kuna uwezekano kwa waandishi wa habari kupata baadhi ya picha pamoja na video ukilinganisha na hapo jana ambapo hakuna aliyeweza kufanya hivyo.
Jambo la pili ni kwamba wiki ijayo, April 19, 2018 kutakuwa na sherehe kubwa huko huko Mombasa lakini inatarajiwa watu wachache ndio wataalikwa na baada hapo itafanyika sherehe nyingine hapa Bongo nyumbani kwa Alikiba, Tabata, Dar es Salaam.
Nne; inaelezwa kuwa katika sherehe ambayo itafanyika Tabata ndipo Alikiba atahamia katika mjengo wake mpya ambao nao umefanywa siri hadi kukamilika kwake.
Tano; Taarifa zinadai mama mzazi wa Alikiba alimueleza mwanae hatoweza kuhamia katika mjengo huo hadi pale atakapokuwa ameoa.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: