Wednesday, 11 April 2018

Makonda: Wanaume Watakaogoma Kuja Mimi Ntaenda Kuwakamata


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amefunguka na kuweka wazi kuwa kuanzia kesho April 12 viongozi mbalimbali wataanza kusambaza barua pamoja na kuwapigia simu wababa ambao wameshtakiwa na wanawake kutelekeza watoto na kusema ambao watagoma kufika ofisini kwake yeye atawakamata.
 
Paul Makonda amesema hayo alipokuwa akiongea na umati mkubwa wa mama ambao wamefika ofisini kwake na kusema kwa siku mbili hizi tayari wameshaweza kusikiliza wanawake zaidi ya elfu moja mia nne na kuwataka wamama hao wamepofika ofisini kwake wawe huru na kuongea mambo yote wasiogope wala kupangiwa mambo ya kuzungumza.

"Wale watakao itwa na wakakaidi kuja mimi nitakwenda kuwakamata kwa hiyo wababa niwaombe tu tusipimane ubavu, msipime nafasi yangu kama ina nguvu au haina nguvu na wale wanaotaka mambo ya siri tunza mwanao ndiyo siri pekee, wewe umetelekeza watoto wamejaa mtaani, wengine wamekuwa ombaomba, wengine wanapelekwa vituo vya vya watoto yatima wakati wazazi wake wapo halafu unajidai kwa akili zako timamu hili jambo la falagha una akili sawasawa kweli? alihoji Makonda

Aidha Makonda amesema kuwa kwa jana na juzi watu maarufu ambao hawataki kuguswa na watu wenye heshima zao tayari wamefika mia moja na saba, Makonda amedai kuwa wapo watu kati ya hao 107 wamekuwa wakihitaji kukutana naye chemba au waje ofisi kwa nafasi za pekee hivyo amesema kuwa hataki kukutana na mtu yoyote chemba wala kupigiwa simu bali wanapaswa kufika ofisini kwake.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: