Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia - Pro. Joyce Ndalichako.

Taarifa ya CAG imeonesha kuwa makusanyo ya mikopo iliyoiva ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilikuwa kati ya asilimia 32 na 48 kwa kipindi cha mwaka 2012/2013 hadi 2016/2017.

Pia taarifa inaonesha kuwa kuanzia mwaka 2015/2016 hadi 2016/2017 makusanyo yaliongezeka kutoka shilingi bilioni 28 hadi bilioni 116 ikilinganishwa na kipindi cha kati ya mwaka wa fedha shilingi bilioni 15 hadi shilingi bilioni 22.

Ongezeko hili la mwaka mmoja ni zaidi ya asilimia 300. Pamoja na mafanikio hayo yanatoka na jitihada kubwa inayofanywa na Menejimenti ya Bodi ya Mikopo, CAG ameonesha kuwa bado kiwango cha urejeshwaji hakiridhishi kutokana na kutokuwepo kwa mikakati thabiti ya ukusanyaji wa madeni ya mikopo.

Serikali inaendelea kuimarisha mikakati yake ya ukusanyaji madeni ya mikopo ambapo kwa mwaka wa fedha 2017/2018 hadi kufikia mwezi Machi 2018 jumla ya shilingi bilioni 132.30 zilikuwa zimekusanywa.

Kiasi hicho cha fedha ni sawa na asilimia 101 ya lengo la mwaka 2017/2018 ambalo ni shilingi bilioni 130. Makusanyo ya mwaka 2016/17 yalikuwa ni shilingi bilioni 116.



Imeandaliwa na Idara ya Habari - MAELEZO
Share To:

msumbanews

Post A Comment: