Monday, 16 April 2018

Majay amwambia Lulu, ‘Utaendelea kuwa wa muhimu kwangu’

Mkurugenzi Mtendaji wa E FM, Francis Anthony Ciza a.k.a Majay ambaye anayetajwa kuwa mpenzi wa wa Elizabeth ‘Lulu’ Michael amesema mrembo huyo ambaye anatumikia kifungo cha miaka miwili jela ataendelea kuwa mtu wa muhimu kwake.

Ujumbe wa Majay unakuja ikiwa leo, April 16, 2018 ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake Lulu. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Majay ameandika;
There are many days passing in life, but today is very important. First it explains that you are a very important person in your life, and second; You continue to be the most important person to me. You are a Woman and a half. I love you so much, Mama G. Happy birthday.
Tetesi za mahusiano ya Majay na Lulu zilishika kasi zaidi baada ya wawili hao kuongozana kwenda Nigeria katika utoaji wa Tuzo ya Africa Magic Viewers Choice (MVCA),mwaka 2016.

November 13, 2017 Elizabeth ‘Lulu’ Michael alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua aliyekuwa muigizaji mwenzake, Steven Kanumba bila kukusudia.

Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: