Mahakama yafungia rasmi mtandao wa TelegramMahakama mjini Moscow nchini urusi imekubali ombi kutoka kwa Mamlaka ya Vyombo vya Habari nchini humo kufunga mtandao wa Telegram haraka iwezekanavyo.

Mamlaka hiyo ilifanya ombi la kufungwa kwa mtandao huo kutokana na kampuni ya mtandao huo kukataa kutoa taarifa zinazotumika kufungua jumbe za watumiaji.

Wakala wa Ulinzi nchini humo FSB wameeleza kuwa Telegram imetumika katika kutekeleza matukio ya kigaidi nchini humo Urusi ikiwa ni pamoja na tukio la bomu lililoua watu 15 katika eneo St. Petersburg la mwaka jana.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: