Mahakama ya  Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, hali ya Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva ni mbaya (very Serious), na amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Kufuatia hali hiyo, mahakama jana ilishindwa kuwasomea maelezo ya awali (PH)  rais huyo Simba ambaye anashtakiwa pamoja na makamu wake, Godfrey Nyange maarufu kama Kaburu.

Kesi imeahirishwa baada ya Mwendesha Mashtaka kutoka Takukuru, Leonard Swai kueleza mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa Aveva ni  mgonjwa (very Serious)  amelazwa katika hospitali ya Taifa  ya Muhimbili.

Swai aliomba mahakama iipangie kesi hiyo tarehe nyingine wakati wakisubiri afya ya Aveva iimarike.

Hakimu Simba aliutaka upande wa mashtaka kuhakikisha unaandaa maelezo ya awali, ili tarehe inayokuja waweze kusomewa PH na siku ikianza kusikilizwa, isikilizwe mfululizo. Kesi imeahirishwa hadi Aprili  25/ 2018.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi na kutakatisha fedha dola za kimarekani 300,000.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: