Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) Mkoa wa Temeke imetaja Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Mahakama, Polisi na Sekta Binafsi kuongoza kwa kulalamikiwa zaidi kwa vitendo vya rushwa dhidi ya wananchi ambapo jumla ya taarifa na malalamiko 232 ziliwasilishwa kwao
Akizungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Takukuru Temeke Bi. Pilly Mwakasege amesema taarifa hizo ni zakipindi cha mwezi Oktoba mwaka 2017 hadi  Machi  2018 ambapo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imekuwa na malalamiko 87, Mahakama 37 na Malalamiko 26 ni ya Jeshi la Polisi ambapo malalamiko yote yameshughulikiwa na kesi kupelekwa Mahakamani.
Pamoja na hayo ofisi hiyo imeweka wazi kuwa Takukuru imeweza kuokoa zaidi ya shilingi milioni 44 kutoka kwa mishahara hewa, mfuko wa jimbo, malipo ya zabuni kwani wanasiamamia fedha zote za miradi ya maendeleo na kuwahimiza Wananchi kuendeleza ushirikiano na mamlaka hiyo katika kudhibiti vitendo vya rushwa.
Aidha, Mwakasege amesema wanaendelea kutoa elimu ya umma kwa lego la kuwaelimisha Wananchi Juu ya Haki na Wajibu wao katika kupambana na rushwa, kuwaelewesha njia za kuwasilisha malalamiko na kutoa elimu ya uelewa wa masuala ya rushwa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: