Friday, 27 April 2018

Magari yaliyokuwa yamebeba Wanajeshi na Polisi yapata ajali Morogoro

Basi lililokuwa limebeba polisi limegongana na gari dogo aina ya Noah iliyokuwa imebeba Wanajeshi wa JWTZ, katika maeneo ya Bwawani mkoani Morogoro.
Imeelezwa kuwa Basi hilo la Polisi lilikuwa likitokea jijini Dodoma kwenye sherehe za Muungano zilizofanyika jana Aprili 26, 2018 huku Noah hiyo iliyokuwa na Wanajeshi takribani 6 pamoja na mtoto ikitokea Morogoro.
Hata hivyo, bado hakuna taarifa ya vifo kwenye ajali hiyo na Kamanda wa Polisi, Ulrich Matei amesema atatoa taarifa za kina baaadae.

Kupata habari zaidi bonyeza link hapo chini.

No comments:

Post a Comment