Posted On: April 25th, 2018
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto ( MTAKUWWA) yaliyotolewa kwa  wajumbe wa kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,mkurugenzi wa Halmashauri hiyo  Ndg. Christopher J. Kazeri amesema mafunzo hayo ni muhimu na kusisitiza kuwa wanawake na watoto mbali na kupata ulinzi wanahitaji kufahamu namna ya kujikinga/kujihami na ukatili na unyanyasaji pia amewataka wajumbe hao kufikisha mafunzo hayo kwa wengine hivyo mafunzo hayo kufikia jamii kwa upana .
Happiness Mugyabuso ambaye ni mchumi kutoka ofisi ya Waziri mkuu amesema mpango wa taifa wa miaka mitano  kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto unalengo la kuhakikisha ifikapo 2021 ukatili dhidi ya wanawake na watoto uwe umepungua kwa asilimia 50, hivyo ili kufikia lengo hilo amewasihi wajumbe kuhamasisha ,kuelimisha jamii kuacha mambo yanayo sababisha ukatili na unyanyasaji wa wanawake na watoto na kuwa tayari kutoa msaada wa kuwanusuru na wanawake hao na watoto.
Mchumi Happiness ameeleza mpango huo  wa taifa utakapotekelezwa ipasavyo utaimarisha kipata na kuongeza idadi  ya wanawake kumiliki mambo mbalimbali ikiwemo ardhi.
Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la John Snow Inc (JSI)  ambalo linatekeleza mradi wa mpango wa uimarisha ji wa mfumo wa afya na ustawi wa jamii (CHSSP) unaofadhiliwa na USAID Ndg.Antony Mwendamaka amesema utekelezaji wa mradi wenye lengo linaloendana na la taifa na kimataifa  kwenye mkoa wa Arusha umetekelezwa kwenye Halmashauri mbili na kwa sasa utatekelezwa kwenye Halmashauri ya meru
Nae Afisa ustawi wa  jamii Halmashauri ya Meru Restuta mvungi ameeleza mafunzo hayo yataongeza nguvu kwenye kutekeleza majukumu ya kitengo cha ustawi wa jamii pia amepongeza mpango wa taifa wa kupambana na ukatili na unyanyasaji wa wanawake na watoto (MTAKUWWA) ambao umeboreshwa kwani wajumbe waliopo wanauhusiano wa karibu na wanawake na watoto akituo mfano wa walimu (maafisa elimu)ambao mpango huu unawatambua kama wajumbe.
Mafunzo haya yenye lengo la  kuwaweshesha wajumbe wa kamati za (MTAKUWWA) ngazi za wi kuwa na uwezo wa kuratibu afua mbalimbali kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto yameandaliwa na ofisi ya Raisi TAMISEMI,Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee ,Wanawake na Watoto kwa kushirikia na shirika lisilo la kiserikali la JSI yatafanyika kwa siku tatu kuanzia leo tarehe 25 Aprili hadi 27 Aprili 2018.
Ndg.Happiness Mugyabuso ambaye ni mchumi kutoka ofisi ya Waziri mkuu akieleza lengo la mradi wa taifa wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na vijana (MTAKUWWA)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg. Christopher J. Kazeri  akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mpango wa Taifa wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto yaliyotolewa kwa  wajumbe wa kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali JSI Ndg.Antony Mwendamaka akielezea mradi (CHSSP) unaotekelezwa na shirika lake la JSI
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakifuatilia kwa makini mafunzo  ya mpango wa Taifa wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakifuatilia kwa makini mafunzo  ya mpango wa Taifa wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto
mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Patandi (jina limehifadhiwa)akifuatilia kwa makini mafunzo  ya mpango wa Taifa wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto
Baadhi ya maafisa ustawi wa jamii wakifuatilia kwa mafunzo ya mafunzo  ya mpango wa Taifa wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto
Share To:

msumbanews

Post A Comment: