Thursday, 5 April 2018

Madiwani wa Chadema Arusha wamkataa Mkurugenzi wa Jiji


Diwani wa chadema Arusha wa Kata ya Ngarenaro  Isaya Doitha Apingana na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athumani Kihamia.

Hayo yamejiri leo katika kikao cha kamati ya fedha ya Jiji ambapo diwani huyo alipinga vikali Mkurugenzi kwa kueleza kuwa Mkurugenzi wa Jiji hatoi ushirikiano dhidi ya madiwani wa chama cha demokrasia na maendeleo.

"Mimi kama diwani wa kata ya Ngarenaro nakueleza wazi hauna ushirikiano na madiwani wa chadema ambapo sisi ndio tunaongoza jiji  na ikiwezekana Rais akuondoe  jijini hapa kwa kuwa tangu umekuja  hakuna kazi unayoifanya kwa kushirikiana na sisi na unafanya kwa utashi wako mwenyewe  kwa kuwa wewe ni mkurugenzi  kwa sababu hiyo waheshimiwa madiwani wenzangu naomba mniunge mkono kwa hili kikao kijacho tumkatae kabisa huyu Mkurugenzi".Alisema Diwani Isaya Doitha

Pakua App yetu ili uweze kuhabarika zaidi

Tumekurahisishia; 
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: