Friday, 27 April 2018

Lipuli yakanusha Salamba kujiunga Yanga

Uongozi wa Lipuli FC umekanusha taarifa zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwamba mchezaji wao Adam Salamba atajiunga na Yanga kwa ajili ya msimu ujao 2018/17.
Afisa habari wa Lipuli Clement Sanga kupitia Azam TV amewaambia mashabiki wa timu hiyo kuzipuuza taarifa hizo.
“Tangu tumemaliza mechi yetu dhidi ya Simba, kumekuwa na taarifa zinazomhusisha mchezaji wetu nyota Adam Salamba kwamba anatakiwa na Yanga kwa ajili ya msimu ujao wa 2018/19.”
“Sisi hatuna taarifa rasmi kutoka Yanga ambayo inaonesha kumtaka Salamba.”
“Kwa namna soka lilivyo duniani huwezi kumzuia mchezaji kutoka klabu moja kwenda nyingine, kama vilabu vinavutiwa na mchezaji kutoka klabu yetu tunachosisitiza ni kufuata sheria kanuni na taratibu zinazotawala mchezo wa soka ili kuondosha migogoro isiyo ya lazima.”

No comments:

Post a Comment