Friday, 20 April 2018

LIPULI WAPANGA KUVUNJA REKODI YA SIMBAUongozi wa Lipuli FC umesema tayari umeshakamilisha maandalizi ya kuingamiza Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kesho.

Lipuli itakuwa kwenye dimba lake la nyumbani mjini Iringa ikiikaribisha Simba ambapo mtanange huo utaanza majira ya saa 10 kamili jioni.

Msemaji wa timu hiyo, Clement Sanga, ameeleza kuwa tayari wameshajipanga na amewahiidi Simba wajiandae kupokea kichapo cha mabao si chini ya mawili.

Kikosi hicho kimeshamiria kuivunja rekodi ya Simba ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja toka msimu huu wa ligi 2017/18 uanze.

Simba itaingia dimbani ikiwa na alama 58 kileleni na ikiwa na njaa ya kuukosa ubingwa wa ligi kwa takribani misimu zaidi ya minne. 
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: