LENGO LA SIRI" SURA YA KWANZA


Mwandishi: Innocent Makauki

Clock tower street 03:45 Arusha
Shughuli zilionekana kuendelea kama kawaida.

Siku ya jumamosi iliyoanza na hali ya hewa ya baridi kali utadhani friji zote mjini zimeachwa milango wazi. Siku iliyokua imenuna na ukungu mzito uliotanda angani uliokua ukifanya uwezo wa kuona mbele usizidi mita kumi na zaidi.

Ndani ya jiji hili ulikua ndo msimu wa utalii unaanza kukolea "high season" magari ya kubebea watalii aina za shuttle mini busses na land cruiser long busses yalikua ndio yanayoziremba barabara za Arusha na viunga vyake.

Katika barabara hii, fly catchers walikua nao kazini tayari, hawa huranda hapa na pale kutafuta watalii wapitao kwa miguu na kuangalia namna ya kujipatia kipato.

Utasikia tu "hello Madame welcome to Arusha", "Hello i have the tour company for you" ilimradi kueza kumvuta mtalii na kufanya nae kazi.

Maduka ya vinyago, nguo za asili, migahawa ya kihindi, kijapani na hoteli nzuri ndio aina za biashara zilizouremba mtaa huu huku katika vibaraza vyake  vilivyoungana pembezoni mwa barabara watu walikua wakipita kuelekea makazini, biashara ndogondogo kama vijimeza vya wauza magazeti na mchinga wadogowadogo zilikua zishafunguliwa.

Job Steven alikua ni miongoni mwa watu waliokua wakitembea pembezoni mwa vibaraza hivi akijikinga na manyunyu ya mvua yaliyokua yanaanza kushuka yakiambatana na upepo kidogo uliozidi kuikoleza baridi iliyokuepo.

 Job alivalia sweta zito la kijivu na koti refu jeusi juu yake, skafu ya sufi na jeanz nyeusi mwonekano uliokua haumtofautishi sana na watu wengne kwani kila aliyepishana naye alikua amejiandaa vizuri kwa hali ya hewa iliyokuepo.

Ungefikiri ni pale kwenye viunga vya Texas marekani msimu wa baridi kali kwa muonekano wa watu na hali ya hewa pia na sura za wageni wa kizungu zilizokua zikionekana hapa na pale.

Job akaamua asimame kidogo kwenye kibanda cha magazeti akiitupia macho saa yake ikiwa ni bado dakika kumi tu kufika nne asubuhi.

Akaagiza sigara aina ya Embassy filter akaiwasha kisha  akatupia macho kwenye vichwa vya habari vya siku hiyo ikiwa ni Ijumaa ya tarehe 30 mwisho kabisa mwa mwezi wa sita.

Magazeti mengi yalijaa habari za kisiasa udaku. Itaendelea Kesho...
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: