Monday, 30 April 2018

Kocha wa Liverpool ajiuzulu


Timu ya Liverpool itamaliza msimu bila ya kocha msaidizi, kutokana na kocha huyo Zeljeko Buvac kujiuzulu nafasi yake baada ya kutofautiana na kocha mkuu wa klabu Jurgen Klopp.

Taarifa hiyo imekuja ikiwa zimebaki siku chache kabla ya mchezo wa marejeano wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya klabu ya AS Roma siku ya jumatano nchini Italy.

Hakuna taarifa rasmi kutoka katika klabu ya Liverpool kuhusu chanzo cha kujiuzulu kwa kocha huyo lakini vyanzo mbalimbali vinadai kwamba siku za hivi karibuni Buvac amekua hana mahusiaono mazuri na Klopp.

Kwa upande wa taaarifa ya klabu ya Liverpool imesema Buvac bado ataendelea kuwa mfanyakazi wa timu hiyo bila kueleza chanzo cha kujiuzulu kwake.

No comments:

Post a Comment