Sunday, 15 April 2018

Klabu ya Barcelona yaweka rekodi mpya La Liga

Klabu ya Barcelona jana usiku imeweka rekodi mpya nchini Hispania baada ya kuchomoza na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Valencia kwenye mchezo wa Ligi kuu nchini humo La Liga.
Barcelona inakuwa klabu ya kwanza kucheza michezo mingi (39) bila kupoteza kwenye La Liga na kuvunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na klabu ya Real Sociedad ya kucheza michezo 38 bila kupoteza rekodi ambayo iliwekwa msimu wa 1979/80.
Kwa sasa Barcelona wanaongoza ligi kwa alama 82 mbele ya Atletico Madrid wenye alama 68 na Valencia wapo nafasi ya tatu na alama 65.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: