Kitwanga: Ukiwa msema Ukweli lazima wakuondoe


Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga amefunguka na kusema kuwa mtu ukiwa msema ukweli lazima wakuondoe katika nafasi yako kwa kuwa hawataki watu wasema kweli.

Kitwanga amesema hayo bungeni alipokuwa akichangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2018/2019, mjini Dodoma na kudai hata ukiwa mtenda haki kwa kila mtu lazima wakuhamishe.

"Kichwa changu na kichwa cha Jenista Mhagama ni vichwa viwili tofauti kabisaa na uwezo wetu wa kufikiri upo tofauti kabisaa, kwa hivyo ni vyema tukapima na kuhakikisha kwamba pale anapofaa Jenista Mhagama aende Jenista Mhagama, pale anapofaa Kitwanga aende Kitwanga lakini hii ya kubebe jumla jumla na wakati mwingine ndugu zetu hii tabia ife na mimi siwezi kukubaliana na hilo na bahati nzuri ukiwa msema ukweli hata ukikaa pazuri watakuondoa tu. Na ukiwa unatenda haki kwa kila mtu hata ukikaa Kolomije watakuondoa wakupeleke Mtwara" alisisitiza Kitwanga

May 21, 2016 Mh Charles Kitwanga, alitenguliwa nafasi yake kama  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa sababu ya kuingia bungeni na kujibu swali linalohusu wizara hiyo akiwa amelewa.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: