Kichuya : Hakuna timu itakayotuzuia kuchukua ubingwa msimu huu - MSUMBA NEWS BLOG

Thursday, 12 April 2018

Kichuya : Hakuna timu itakayotuzuia kuchukua ubingwa msimu huu


Kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya

BAADA ya kufanikiwa kuwafunga Mtibwa Sugar, kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya ameweka wazi kuwa kwa sasa hakuna timu itakayowazuia kuchukua ubingwa wa msimu huu kwa kuwa mechi hiyo haikuwa ya kawaida.

Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa katika mchezo uliopigwa juzi Jumatatu kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. Ushindi huo umepelekea Simba kuende­lea kuongoza ligi kwa pointi 52, nyuma ya Yanga yenye pointi 46.

Akizungumza Kichuya alisema kuwa kwa sasa haoni timu ambayo inaweza kuwazuia kuchukua ubingwa baada ya kufanikiwa kuifunga Mtibwa.

“Binafsi kwangu ni jambo la furaha kufanikiwa kushinda dhidi ya Mtibwa kwa sababu hii mechi haikuwa rahisi kwetu na tulikuwa tunahitaji matokeo mazuri ili kufikia malengo.

“Kiukweli Mtibwa wamecheza vizuri na mchezo ulikuwa mgu­mu lakini kwa matokeo haya sioni timu ambayo itaweza kutuzua kuchukua ubingwa wa msimu kwa sababu tunapam­bana bila ya kuangalia nyuma anakuja nani,” alisema Kichuya.
Comments


EmoticonEmoticon

Notification
This is just an example, you can fill it later with your own note.
Done