Thursday, 19 April 2018

KIBAHA SEKONDARI KINARA WA INSHA, SHULE NYINGINE ZATAKIWA KUJIFUNZA KUTOKA KWAO

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Ave Maria Semakafu amezitaka Shule za Sekondari nchini ambazo zimekuwa zikishindwa katika mashindano ya insha za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika SADC kujifunza kupitia shule ambazo zimekuwa zikifanya vizuri.

 Dkt. Semakafu ameyasema hayo mjini Dodoma wa wakati hafla ya kuwazawadia washindi wa insha hizo kwa mwaka 2017 ambapo amesema ni vema kukawa na  utaratibu wa kuzikutanisha shule hizo mara moja kwa mwaka ili kujadiliana mbinu mbalimbali zitakazowawezesha kufanya vizuri katika mashindano hayo
Semakafu amesema ushindi huu ni dhahiri kuwa Elimu  inayotolewa nchini  ni Elimu bora na diyo maana wanafunzi wa kitanzania wameweza kushinda tuzo na kuongoza  katika ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Nchi za kusini mwa Afrika.

 Afisa Elimu Mkuu wa sekretaieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki James Otieno kauli ailiunga mkono  kauli hiyo kwa kusema kuwa Elimu nchini Tanzania ni bora kwa Nchi za ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwsababu wanafunzi kutoka Tanzania wamekuwa wakifanya vizuri katika mashindano hayo.

Kwa upande wake Mwanafunzi bora wa mashindano ya insha hizo kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Michael Msafiri kutoka Shule ya Sekondari Kibaha ndiye atakuwa mwakilishi wa washindi wote katika Mkutano Mkuu wa Wakuu wa nchi za Jumuiya hiyo utakaofanyika baadae mwaka huu mkoani Arusha.

Kaimu Mratibu wa mashindano hayo Salum Salum kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia amesema mshindano haya huanza mara baada ya kikao cha wakuu wa Nchi wanachama kutoa azimio la mwaka na kwamba mada zinazoshindanishwa huzingatia makubaliano ya wakuu wa nchi.

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI, NA TEKNOLOJIA.
18/4/2018


Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: