Wednesday, 4 April 2018

Keai ya Wema sepetu dhidi ya madawa April 23


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajiwa kutoa maamuzi kuhusu kesi ya matumizi ya madawa ya kulevya inayomkabili Muigizaji Wema Sepetu, Aprili 23 mwaka huu.

Mahakama hiyo inatarajiwa kutoa maamuzi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi watano wa upande wa mashtaka na kuanika iwapo Wema Sepetu na wenzake wawili kama wana kesi ya kijibu au la.

Wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Angelina Msigwa na Matrida Seleman Abbas ambao wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.

Wema Sepetu ni moja ya wasanii ambao waliwahi kutajwa katika orodha ya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda ya watu wanaohusika na kutumia au kuuza dawa za kulevya Februari 06, 2017.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: