Saturday, 28 April 2018

KAULI YA JOHN HECHE BAADA YA MDOGO WAKE KUUAWA NA POLISI


Saguta Chacha enzi za uhai wake.

KUFUATIA kifo cha mdogo wake aitwa Saguta Chacha, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amelishutumu Jeshi la Polisi kwa kusababisha kifo hicho huku akisema si mara ya kwanza kwa familia yao kukutana na mikasa kama hiyo.

Saguta anadaiwa kuuawa baada ya kuchomwa kisu na askari polisi baada ya kuibuka ugomvi wakati alipokuwa akipelekwa kituo cha polisi baada ya kukamatwa ambapo RPC wa Mara alithibitisha kutokea kwa tukio hilo jana.

Heche amesema;
Mpaka sasa sielewi ni kwa vipi mtu anaweza kuuawa na polisi kwa kuchomwa kisu tena akiwa amefungwa. Kuchoma mtu kisu mgongoni ni kudhamiria kuua kwasababu hakua hata anapambana. Nilijua mikononi mwa polisi ni sehemu salama.

Wiki mbili zilizopita kijana Allen alikufa katika maizingira tata kule Mbeya, Mwanza mama aliakamatwa na kunyimwa dhamana, mtoto wake mchanga alikufa.
Leo ni kwangu mdogo wangu ameuwawa kikatili sana mikononi mwa polisi. Maisha yangu yote nimeyatoa kupigania haki ili watu wasionewe, mtuhumiwa asifanywe mkosaji na kuhukumiwa kabla ya vyombo vya sheria kumhukumu.

Mwaka jana mdogo wangu mwingine aliumizwa vibaya sana na polisi. IGP Mangu na RPC aliyekua Tarime walilipa uzito suala hilo lakini alipoondolewa, suala liligeuzwa kisiasa na wale vijana waliokua wamemjeruhi mdogo wangu ambae mapaka sasa sikio moja halisikii, wakarudishwa kazini kinyemera na kuhamishwa Tarime kama kunikomoa.

Mimi nimewahi kutishiwa kuuawa kituo cha polisi, najisikia maumivu makubwa mno lazima Watanzania wakatae hali hii. Waziri yuko kimya, wangapi wanakufa na kuumizwa mikononi mwa polisi bila matukio kujulikana wala kutangazwa?
Nitazungumza mda ukifika. Amesema John Heche, Mbunge Tarime Vijijini (Chadema).

No comments:

Post a Comment