Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe amefunguka na kukiri wazi kuwa hakuweza kwenda ofisi za uhamiaji kwa mara ya kwanza alipoitwa kutokana na kuwa busy na shughuli za pasaka.
Mchungaji Kakobe amesema hayo baada ya kupata wito wa pili kufika katika ofisi za uhamiaji siku ya Jumatatu April 9, 2018 ambapo amesema kuwa atakwenda ili kuitika wito huo kama ambavyo amehitajika kufika majira ya saa nne asubuhi. 
"Ni kweli tumepata barua ndiyo tunajipanga kwenda kesho Jumatatu majira ya saa nne asubuhi kama ambavyo barua imedai, ni kweli niliitwa kwa mara ya kwanza ila yalikuwa ni majira ya pasaka na kipindi hicho kidogo tulikuwa na shuguli nzito kwa ajili ya sikukuu ya Pasaka ambayo ndiyo sikuu kubwa sana kwa wakristo, kwa hiyo kutokana na kutofika ndiyo maana wameleta hii barua nyingine ya kukumbushia hivyo tutafika hiyo kesho kutokana na wito wao" alisisitiza Kakobe 
Kwa upande wa Naibu Kamishna wa Uhamiaji Crispin Crispin Ngonyani alikiri kumwita kwa mara ya pili mchungaji huyo lakini hajaweza wazi sababu kubwa za wao kumwita mchungaji huyo katika ofisi zao, ingawa watu wanahusisha kuitwa kwa Kakobe kuwa huenda ofisi hizo zina mashaka na uraia wake kama zilivyo onyesha mashaka juu ya uraia wa Mwanafunzi wa UDSM Abdul Nondo ambaye amehitajika kufika ofisi za uhamiaji tarehe 20 April akiwa na vyeti vya kuzaliwa vya wazazi wake wote, pamoja na vyeti vya babu na bibi zake wa pande zote za wazazi wake.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: