Saturday, 14 April 2018

JULIO:SASA NIPO TAYARI KUCHUKUA NAFASI YA LWANDAMINA


Na George Mganga

Kocha wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema kuwa aliwahi kuharibiwa mipango ya kujiunga na Yanga ili kuchukua nafasi ya ukocha wakati Abbas Tarimba akiwa ni mmoja wa viongozi ndani ya timu hiyo.

Julio ameeleza kuwa aliwahi kufanyiwa umafia na baadhi ya watu ambao walikuwa hawampi nafasi ya kupata nafasi hiyo.

"Niliwahi kupata nafasi Yanga ili niwe Kocha, lakini kuna baadhi ya watu waliokuwa hawana nia njema wakati Abbas Tarimba akiwa kiongozi waliniharibia mipango" amesema Julio. 

Mbali na hilo, Kocha Julio amesema yupo tayari kuinoa Yanga ambayo imeondokewa na Kocha wake Mkuu, George Lwandamina, aliyerejea kujiunga na timu yake ya zamani, Zesco United, nchini Zambia.

kwa mujibu wa E Sports kutoka EFM, Julio anaamini anaweza kuifundisha Yanga kutokana na uzoefu alionao ndani ya soka la Tanzania sababu akieleza ameshafundisha baadhi ya timu hapa nchini.

"Nipo tayari kufundisha kama watakubaliana namimi, nina uzoefu wa kutosha katika kazi hii" amesema. 
  

Yanga hivi inajiandaa na safari ya kesho kuelekea Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa pili ambao ni wa marudiano dhidi ya Wolaitta Dicha FC.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: