Monday, 30 April 2018

John Heche afunguka mpaka sasa hawajaamua juu ya mazishi ya mdogo wao


Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche ambaye pia ni kaka wa marehemu Chacha Heche Suguta, amesema kwamba mpaka sasa hawajaamua juu ya mazishi ya mdogo wao, ambaye aliuawa na Polisi

Akizungumza na www.eatv.tv. Mheshimiwa Heche amesema kwa sasa wapo kwenye kikao cha familia wakijadili juu ya suala hilo, na watakapopata suluhu ya kuzika ama la, wataujulisha umma.

Chacha Suguta aliuawa Ijumaa ya April 27 kwa kuchomwa kisu na polisi wa kituo cha Sirari, waliokuwa wamemkamata baada ya kumkuta bar akinywa pombe.

No comments:

Post a Comment