Saturday, 14 April 2018

JOHARI: NITAENDA KWA MAKONDA KUSEMA NIMEACHWA


Blandina Chagula ‘Johari’
MUIGIZAJI mkongwe kwenye tasnia ya filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ ametoa kali ya mwaka baada kusema kuwa na yeye atakwenda kwenye Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kudai kuwa ameachwa wala sio kutelekezewa mtoto au kunyimwa matunzo ya mtoto.

Akizungumza na Risasi Jumamosi Johari alisema, yeye hana shida ya kuachiwa mtoto bali ataenda kusema kuwa aliachwa na mtu ambaye alikuwa akimpenda hivyo aangalie utaratibu ambao na yeye atasaidiwa kama mwanamke aliyeachwa.

“Mimi nitaenda pale lakini tatizo langu ni tofauti kabisa maana mimi ni kuhusiana na kuachwa tu na si vinginevyo” alisema Johari ambaye hakumtaja mtu anayemlenga licha ya kwamba aliwahi kuwa kwenye uhusiano na staa wa filamu, Vincent Kigosi ‘Ray’.

Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: