JINA LA RIWAYA: LENGO LA SIRI (COVERT PURPOSE)


MWANDISHI: INNOCENT MAKAUKI
INSTAGRAM: Makeynovels_tz
MOVIE SCRIPS: 0622088300

Inaendelea ilipoishia toleo lililopita.....

SEHEMU YA TATU.

Job akaamriwa na kuanza kutembea huku akiwaza ni jinsi gani alichokitarajia kimegeuka kua dunia nyingine kabisa.
 Kwani ni masaa kadhaa tu yamepita simu yake ya mkononi ilipoita akiwa amejilaza kwa uvivu wote kitandani baada ya shughuli nzito ya usiku kucha na huyu mrembo Naomi aliyelala pembeni yake akiwa amefunika tu sehemu ya kiuno ya mwili wake. Kuzungumzia tu umbo kwa alivyokua amejilaza kwa mgongo basi kila silaha alikua nayo. Job alijisogeza na kuutoa mkono wa Naomi kifuani mwake na kuichukua simu mezani huku mrembo akilalamika kwa minong'ono ya kusumbuliwa, akapokea simu bila kuangalia ni nani anayepiga.
"HALLO"
Upande wa pili kimya
"HALLOO" Job akaita tena kwa sauti isiyokua ya kivivu tena, yenye msisitizo kidogo.
"IS THIS JOB?" Wakati huu upande wa pili ulijibu. Sauti nzito ya kiume iliyojaa kila aina ya hofu iliuliza kwa lugha ya kiingereza. Job akaamka na kukaa akiisikiliza kwa makini kwani haikua simu ya kawaida kwake.
"Yes. Who are you?" akauliza
"My name doesn't matter for now. Listen to me carefully" upande wa pili ulisisitiza. Job akaruka nje ya kitanda na kusimama akisikiliza kwa makini. Simu kama hizi hazikua ngeni sana hasa kwa kazi ya ukachero nyingi zimewahi kua za vitisho hasa hasa upelelezi unapogusa kuharibu maslahi ya watu wenye fedha zao ama nyadhifa kubwa kwenye makundi ya kimafia hata serikalini wakati mwingine. Hofu ilianza kumtanda kuanzia tumboni kijasho kidogo puani hata miguu ilikua imesimama ikiwa imepoa kama mtu aliekua katika hatua za mwisho kukata roho, akataka kujibu lakini mdomo ukawa mzito kama ana tonge la ugali mkavu, pumzi ikamkaba kooni huku akimgeukia Naomi alipolala akakohoa kidogo kusafisha koo "Yes I'm listening" akajibu sauti safari hii ikiwa ya chini japo hapo ndipo alipoitoa kadiri ya uwezo wake wote.
"With no doubt you know the tragic accident that led to the death of Prime minister Robert Kabwe three months ago" sauti iliendelea kuongea wakati huu ikiwa imetulia kidogo. Job hakujibu chochote zaidi ya kuendelea kusikiliza.
"You have been working hard undercover to investigate who's behind the accident, and finally shot the minister and his driver in cold blood" .....

Itaendelea Kesho
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: