Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa wilaya ya Ilala Mhe. Sofia Mjema pamoja na watendaji wengine wa serikali wakifanya ukaguzi wa miundombinu iliyoathiriwa na mvua.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali  na wananchi wakiangalia athari za mafuriko katika maeneo ya jiji la Dar es salaam.


 Uharibifu wa daraja la Ulongoni B.
 Uharibifu wa daraja la Ulongoni A
Mto katika Daraja la Pugu Mdadani ukiwa umechepuka na kusababisha wananchi kukosa huduma ya usafiri.
......................................................

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo leo amefanya ziara maalum ya kukagua miundombinu ya barabara za mwendo Kasi eneo la Jangwani pamoja na kukagua uharibifu mkubwa wa madaraja yanayounganisha maeneo mbalimbali katika jiji la Dar es salaam. 

Kutokana na athari aliyoiona katika maeneo ya Pugu, Mnadani na Ulongoni Jafo ameamua kuomba msaada wa haraka kutoka Jeshi la wananchi(JWTZ) kupitia Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Hussein Mwinyi ili jeshi hilo liweze kujenga madaraja ya dharula katika maeneo hayo pamoja na maeneo mengine yaliyopata maafa kama hayo hapa nchini. 

Aidha kutokana na athari hizo, Waziri Jafo amepiga  marufuku uchimbaji wa mchanga katika kingo za mito ili kuzuia mito iliyopo isichepuke. 

"Uchimbaji wa mchanga umechangia maeneo mengi kuanzisha mapito mapya ya maji na kuathiri miundombinu mbalimbali," amesema.

Kwa upande wao, Wakazi wa Ulongoni wameishukuru  serikali kwa kuonyesha uharaka wa kuwapatia ufumbuzi kwani maeneo yao hayapitiki kabisa kwasasa
Share To:

msumbanews

Post A Comment: