Thursday, 19 April 2018

Ikulu yakanusha taarifa alizozushiwa Rais Magufuli


Mkurugenzi wa Mawasiliani ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa amekanusha taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamiii zinazodai kuwa, Rais Dkt John Pombe Magufuli leo  Aprili 19 atazindua Hospitali ya Chanika Dar es Salaam.

Msigwa amesema kuwa, Ikulu haijapanga ratiba hiyo na kwamba wanasubiri taarifa rasmi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto.

Aidha, katika taarifa yake Msigwa alieleza kwamba, kiongozi mwingine yeyote anaweza kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa hospitali hiyo.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: