Thursday, 19 April 2018

Huyu hapa Mke wa Alikiba

 Ikiwa leo April 19, 2018 msanii wa muziki Bongo, Alikiba amemuoa Amina Rikesh, kuna machache ya kukujuza kuhusiana na mrembo huyo.


 Amina Rikesh ni binti wa miaka 23, amezaliwa Kongowea, Mombasa ambapo kwa sasa anafanya kazi ya finacial analyst, kabila lake ni Mmanga.


 Kwa mujibu wa vyanzo vya kimtandao kutoka nchini Kenya, Amina na Alikiba walikutana mwaka 2016.

Baada ya wawili hao kufunga ndoa asubuhi ya leo katika msikiti wa Masjid Ummu Kulthumu ambao ni jina la MamaMzazi wa Gavana wa Mombasa, Hassan Ali Joho, usiku kutafanyika sherehe katika ukumbi wa Diamond Jubilee Hall na sherehe nyingine inatarajiwa kufanyika April 26, 2018 nyumbani kwa Alikiba, Dar es Salaam.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: