SHIRIKA la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) kupitia timu yake ya wataalam wa miundombini wamekabidhi mpango mkakati wa miundombinu ya usafiri kwa lengo la kuondoa msongamano wa magari kwenye Jiji la Dar es Salaam.

Mpango mkakati huo umekabidhiwa leo kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Sipora Liana unahusisha ujenzi wa miundombinu ya usafiri ya aina mbalimbali huku ukitoa mapendekezo ya kujengwa ofisi na masoko pembezoni mwa Jiji hilo ili kupunguza msongamano hasa kwa kuzigatia ifikapo mwaka 2030 kutakuwa na idadi ya watu milioni 10.

Akizungumza leo baada ya kukabidhiwa mpango huo kutoka kwa JICA, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Liana ameahidi kuwa mpango huo utafanyiwa kazi ili kupunguza msongamano unatokana na ufinyu wa miundombinu ya usafiri.

"Timu ya wataala wa JICA  wamefanya utafiti wao na kuja na mpango huu wa miundombinu ya usafiri katika Jiji la Dar es Salaam na kutoa mapendekezo ya mpangilio mzuri wa miundombinu hiyo ili kuhakikisha msongamano unapungua.

"Jiji tunahusika zaidi na mpango huu ambao tumekabidhiwa leo na JICA kwa maana ndio wenye Jiji la Dar es Salaam.Hata hivyo ni mpango ambao utatumia na wadau wote wanaohusika na miundombinu ikiwemo Wizara,"amesema.

Amefafanua mpango huo unazugumzia miundombinu ya usafiri ya aina mbalimbali ikiwemo ya barabara na reli na lengo ni kuhakikisha msongamano unapungua kwani unachangia kukwamisha shughuli za uchumi wa Jiji la Dar es Salaam kutokana na muda mwingi kutumika barabarani.

Ameongeza kuwa "Mpango huo unaenda hadi mwaka 2030 na lazima uheshimiwe na kutekelezwa kama ambavyo mapendekezo yake yanavyotaka".

Pia amesema mpango huo unaonesha namna ambavyo miundombinu katika Jiji la Dar es Salaam inatakiwa iwe na kubwa zaidi wameshauri kuwepo na masoko na ofisi pembezoni mwa Jiji ambazo  zitasaidia wakazi wake kutokuwa na ulazima wa kuinga kati ya mji kwa wingi kufuata mahitaji.

"Ni mpango ambao tumeahidi kuufanyia kazi , unazungumzia namna ambavyo miundombinu ya reli kwa ajili ya usafiri wa treni iweje na iwe kwenye maeneo gani.Ofisi za pembezoni mwa miji nazo ziwe wapi pamoja na mambo mengine mengi yenye lengo la kupunguza msongamano.Mpango huo unaonesha kutakuwa na barabara za juu,"amesisitiza.

Alipoulizwa nafasi ya JICA katika kushiriki kwenye utekelezaji wa mpango huo , Liana amesema JICA ndio wawezeshaji na washauri kuhusu mradi huo ingawa nao  wameshiriki.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: