Picha hapo juu : Ni gari aina ya Fuso Baada ya ya Kupata Ajali hiyo

Ajali ya hii imetokea majira ya saa 20:00 usiku  huko kijiji cha Makomero wilaya ya Igunga Mkoa wa Tabora ambapo Basi  lenye namba za usajili  T.983 DCE mali ya Kampuni ya CITY BOY likiendeshwa na EMANUEL ATUPENDA CHITEMO mkazi likiwa linatokea Ngara Mkoa wa Kagera kuelekea Mkoa wa Dar es salaam   liligongana na  gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T.486 ARB  lilokuwa linaendeshwa na SALUMU ABDALAH KALAMBO na kusababisha vifo vya abiria 12 huku 46 wakijeruhiwa.

 Picha hapo juu: Gari kampuni ya CITY BOY mara baada ya kupata ajali.

 Akiongea na waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Mwandamizi WILBROD MUTAFUNGWA ameeleza kwamba  Abiria 12 walipoteza Maisha huku wengine 46 wakijeruhiwa na kati yao aliwataja abiria watatu ambao hali zao ni mbaya na wawili wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mkoa wa Mwanza na mmoja Nkinga Mission wilaya ya Igunga.

 Kamanda Mtafungwa ameeleza kuwa  chanzo cha ajali hiyo ni Gari aina ya Fuso kupasuka tairi ya mbele upande wa kulia na kusababissha kukatika kwa mfumo wa usukani  likiwa katika mwendo mkali baada ya kuyaingia mashimo mawili yaliyo katikati ya barabara na kusababisha kupoteza mwelekeo na kisha kuligonga basi la abiria lililokuwa likipishana nalo.

Aidha baada ya ajali hiyo dereva wa FUSO alitoweka eneo la tukio na jitihada za kumtafuta zinaendelea
Share To:

msumbanews

Post A Comment: