KWA miaka nenda rudi, udereva ni fani inayoheshimika na wengi. Katika pilikapilika za kila siku, umuhimu wa kazi ya udereva unajidhihirisha waziwazi, ukipanda daladala unamtegemea dereva akufikishe salama, kama una gari lako unategemea dereva afanye kazi yake au kama unaendesha mwenyewe, lazima uwe na ujuzi wa udereva.

Makosa madogo tu ya dereva yanaweza kusaba­bisha madhara makubwa sana, sote tunashuhudia ajali za kutisha zinazogharimu maisha ya watu! Yote hayo ni kwa sababu ya madereva.

Sasa hebu vuta picha, pi­likapilika za maisha ziendelee kama kawaida, magari yaen­delee kutoa huduma bara­barani, daladala ziendelee kupakia na kushusha abiria vituoni, mabasi ya mikoani na yale ya mwendokasi, achilia mbali malori makubwa kwa madogo, yote yaendelee na kazi kama kawaida lakini kusiwe na dereva hata mmo­ja! Ni jambo lisilowezekana si ndiyo?

Basi kwa taarifa yako, ulimwengu wa sayansi na te­knolojia unakwenda kasi mno na huenda miaka ya baadaye, hawa madereva wanaotamba barabarani sasa hivi watalaz­imika kutafuta kazi nyingine kwa sababu kazi hiyo itakuwa imeshafutika kabisa duniani.
Kivipi? Teknolojia im­ewezesha kuvumbuliwa kwa magari yanayojiendesha yenyewe bila kuwa na dereva almaarufu SDC (Self Driving Car) na tayari Kampuni ya Google X ya nchini Marekani na nyingine kadhaa, zinaen­delea kuboresha magari ya aina hiyo.



Majaribio ya magari hayo yalishaanza tangu mwaka 2015 katika barabara za umma kwenye majimbo kadhaa nchini Marekani, yak­iwemo California, Michigan, Florida na Nevada na ma­tokeo yanaonesha kufanikiwa kwa teknolojia hiyo ambayo kwa mujibu wa Google X, itaanza kutumika rasmi dunia nzima mwaka 2020.
Teknolojia inayotu­mika kwenye magari yanayojiendesha yenyewe inafahamika kwa jina la Google Chauffeur. Magari yanayotumia teknolo­jia hiyo, hayatumii mafuta kama magari ya kawaida, badala yake yanatumia umeme.

Mpaka sasa, magari yanayoendelea kujar­ibiwa ni Toyota Prius, Audi TT, Lexus RX450h na magari maalum yaliyotengenezwa na Google kwa kushiri­kiana na Kampuni ya Roush Enterprises. Kinachofanyika ni kwamba kabla gari halijaon­doka, taarifa zake huingizwa kwenye kompyuta kuonesha linaelekea wapi na litapita njia gani mpaka kufika mwisho wa safari yake.

Muongozaji mkuu wa safari za magari yote hubaki kwenye kituo kikuu cha kompyuta za kuongozea magari hayo na hupokea taarifa zote ‘auto­matically’ kuhusu kila gari lililoondoka, mahali lilipo, spidi linayotembea na mambo men­gine muhimu na magari hayo huongozwa kwa kufuata ramani maalum za kampuni ya Google (Google Maps).

Upande wa juu wa magari hayo, kumefungwa kifaa maa­lum kiitwacho Laser ambacho kinatoa mionzi inayowezesha gari kuyatambua mazingira lilipo kwa nyuzi 360, kwa mfano kutambua kwamba mbele, nyuma, kushoto au kulia kuna kitu gani kwa wakati mmoja. Ni rahisi gari kutambua kwamba mbele kuna gari jingine, kuna ajali au kuna taa za kuon­gozea magari hivyo kupunguza mwendo au kusimama inapo­bidi.
Magari hayo huwa pia na kifaa kingine kiitwacho Proces­sor kilichounganishwa na kifaa cha kwanza, Laser ambacho kazi yake ni kutafsiri taarifa zinazotoka kwenye Laser na kulifanya gari kujibadilisha lenyewe kulingana na mahitaji, kama kupunguza mwendo, kufunga breki, kuondoka au kukata kona.
Sensors (position na orienta­tion) ni vifaa vingine vinavyopa­tikana kwenye magari hayo am­bavyo kazi yake ni kuhakikisha gari linakwenda katika uelekeo sahihi na kuelewa limefika se­hemu gani kwa wakati husika.
Upande wa mbele wa magari hayo, kuna kifaa kingine kiit­wacho Radar ambacho kazi yake ni kupima umbali ambao magari mengine yapo na spidi yanayotembea ili kuhakikisha gari linakwenda sawa na spidi ya magari mengine bila kusab­abisha foleni wala kuyagonga magari mengine.

Wakati watu wengi wakione­sha kuifurahia teknolojia hiyo inayotajwa kuwa salama zaidi katika kupunguza ajali zinazo­sababishwa na makosa ya kib­inadamu, madereva wengi wanaonesha kutoiunga mkono teknolojia hiyo kwa kuhofia kupoteza ajira zao.

Changamoto kubwa kwa nchi zi­nazoendelea, itakuwa ni suala la bara­bara kwa sababu ili magari hayo yafanye kazi kwa ufanisi, ni lazima yapite kwenye barabara nzuri za lami, zilizojengwa kwa ramani na kuzingatia ubora wa kimataifa. Ni suala la muda tu ila yajayo yanasisimua sana.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: