Harmonize adai ukimtoa Diamond anafuatia kuwa na nyumba kali kuzidi wasanii wote BongoMsanii wa muziki kutoka label ya WCB, Harmonize amefunguka kuhusu mjengo wake ambao upo mbioni kukamilika
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma ‘Kwa Ngwaru’ ameiambia Funiko Base, Radio Five kuwa mjengo huo upo mbioni kumalizika na utamfanya kuwa msanii wa pili Bongo kuwa na nyumba kali.
“Nasema ukweli mimi nyumba yangu ikiisha, nyumba ninayojenga mimi sijui nitakuwa msanii wa pili wa Dar es Salaam au Tanzania kuwa na nyumba kali, ya kwanza ni Diamond ambayo nayo haijaisha ila ipo katika hatua za mwisho,” amesema Harmonize.
Ameongeza kuwa amefikia mafanikio hayo makubwa kutokana na ushauri mzuri anaopatiwa na mpenzi wake Sarah.
Katika hatua nyingine amefunguka tetesi za mpenzi wake Sarah kuwa na ujauzito na kueleza kuwa hilo halina ukweli ila kwa sasa anaweka mazingira mazuri kwa ajili ya mtoto.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: