Mchezaji wa kimataifa wa Brazil Neymar anatarajiwa kuwa katika afya nzuri kuweza kushiriki katika Kombe la Dunia msimu huu wa joto na anasema atarudi katika mazoezi Mei 17 baada ya kuwa nje kufuatia kuvunjika mguu.
Mchezaji huyo wa kiungo cha mbele wa Paris St-Germain alihitaji kufanyiwa upasuaji mfupa baada ya kujeruhiwa katika mechi ya ligimnamo Februari 25.
Brazil inacheza mechi yake ya ufunguzi dhidi ya Switzerland Juni 17, mwezi mmoja baada ya muda anaotarajiwa kurudi uwanjani.
"Natarajia kurudi nikiwa fiti kabisa," amesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.
Neymar alikuwa mchezaji mwenye gharama ya juu wa soka alipojiunga na PSG kutoka Barcelona Agosti mwaka jana, na amefanikiwa kufungua magoli 25 huku akiwa amesaidia kufanikisha mara 16 kufunga kwa timu hiyo ya Ufaransa msimu huu.
Kwa mujibu wa BBC
Share To:

msumbanews

Post A Comment: