Wednesday, 18 April 2018

Fatma Karume aiomba radhi Serikali

Rais mpya wa Chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS), Fatma Karume ameiomba radhi serikali kwa kutoa lugha kali ambazo zilizokuwa zinaenda moja kwa moja kugusa muhimili wa Mahakama kuhusiana na mambo ambayo yanayoendelea nchini kupitia Mahakama bila ya kufuata haki za kisheria

Fatma Karume ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar ametoa kauli hiyo leo Aprili 18, 2018 wakati akizungumza katika kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio kwa njia ya simu ambapo amesema zoezi la kuteua Majaji nchini liangalie zaidi taaluma za wanaoteuliwa badala ya kuwateua kwa mlengo wa kisiasa.

"Mahakama ni mhimili unaojitegemea hivyo ni vema ukaheshimiwa kwa kuchagua Mahakimu wenye vigezo vya kitaaluma ambao watasimamia vema sheria badala yakuyumbishwa na siasa. Mimi nipo tayari kushirikiana na serikali kwa sababu siwezi kutengeneza bajeti lakini naweza kushirikiana nao katika kuelezea mapungufu yaliyopo", amesema Fatma.

Mbali na hilo, Rais Fatma Karume ameweza kuweka wazi mipango yake ambayo atakayoweza kufanya katika kipindi cha uongozi wake.

"Kitu cha kwanza ni lazima tuifanye Mahakama iweze kufanya kazi zake katika weledi wake kwa hivyo watu wakiwa 'appointed' kuwa Majaji, Mahakimu. Tusiganye hizi 'appointed' kwa mujibu wa siasa lazima ziwe 'professional'. Inamaana kwamba unai-Professionalize Mahakama nzima, hiyo ni 'point' namba 'one' lakini namba mbili mishahara, unajua muda mwingine tunalalamika rushwa lakini unampa mtu laki nane ayaendeshe maisha yake lakini kesi inakuja ya milioni 200 ndani yake, lazima tuweze 'ku-balance' hivi vyote ni vitu muhimu sana maana tunasema tuna muhimili wa Mahakama lakini hatuwezi kujiendesha, hivi kweli muhimili unaweza kusimama? kusimama kwa ari!! na naomba msamaha hapa sababu nasema mambo, unajua saa nyingine unakuwa na hamasa na unaweza kusema mambo ambayo yana 'emotional", amesisitiza Fatma.

Kwa upande mwingine, Fatma Karume amesema kuna madhaifu mengi katika muhimili wa Mahakama ndani ya nchi hii na katika nyanja za sheria ambapo amedai changamoto nyingine ni miundombinu mibovu ya majengo ya Mahakama.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: