Fahamu faida za ulaji wa tunda la nanasi - MSUMBA NEWS BLOG

Sunday, 1 April 2018

Fahamu faida za ulaji wa tunda la nanasi

Nanasi ni moja ya tunda linalotajwa kuwa na faida tele katika mwili wa binadamu licha ya kuwa baadahi ya watu wanadai kuwa tunda hilo si salama kwa akina mama wajawazito, ingawa suala hili bado halijathibitishwa kitaalamu.

Nasasi lina faida nyingi katika afya ya mwanadamu kama vile:- Tunda hil lina vitamini A, B-6 na C, madini ya chuma, calcium, copper na phosphorous ambayo yote ni muhimu sana katika afya ya mwanadamu. Katika mahesabu ya kitabibu, kipande kimoja cha nanasi kinatosha kuongeza 131% ya vitamin C.
Pia tunda hili husaidia kutengeneza damu, kuimarisha mifupa , meno, neva na misuli (muscles),vile vile nanasi lina uwezo wa kutibu matatizo ya tumbo, bandama na ini, husaidia kusafisha utumbo mwembamba, hutibu homa, vidonda mdomoni, magonjwa ya koo, hutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu, hutibu kikohozi, kutetemeka na uoga (Anxiety).

Mananasi pia husaidia mfumo mzima wa usagaji (Mmeng’enyo) wa chakula kwani tunda hilo lina kambakamba (fibre) ambavyo husaidia sana kwenye kusagwa kwa chakula mwilini, kirutubisho cha Bromelain pia husaidia kwenye kusaga chakula tumboni kwa kusaidia kuvunja vile vipande vya protini.
Vitamini C inayopatikana katika tunda hilo husaidia sana kuipa ngozi mng’ao ambao unahitajika, mishipa midogo ya damu pia hufaidika sana kutokana na mananasi pamoja na viungo vingine vya mwili na mifupa pia.
Comments


EmoticonEmoticon

Notification
This is just an example, you can fill it later with your own note.
Done