Thursday, 5 April 2018

Ester Bulaya Naye Kaitwa Polisi Central


Mbunge wa Bunda Mjini kupitia CHADEMA Ester Amos Bulaya, ameitwa kituo cha polisi cha kati jijini Dar es salaam huku akiwa hana taarifa za sababu ya wito huo

Ester Bulaya amesema amepata taarifa za kuitwa kwake polisi kutoka kwa mwanasheria wake na hivi sasa yuko njiani kuelekea kituoni hapo, ingawa hajui kitakachomkuta huko.

“Ni kweli nimepata taarifa kutoka kwa mwanasheria wangu, naitwa kituo cha Polisi na sasa hivi ndio nalekea huko central, sababu za wito huo sijui lakini huenda ikawa kama ya wenzangu kina Mdee”, amesema Ester Bulaya

Hivi karibuni kumekuwa na matukio ya kuwakamata viongozi na wabunge wa CHADEMA na kuwafungulia mashtaka, ambayo baadhi yao wengine wameshapandishwa mahakamani, kwa mashtaka ya kufanya maandamano bila kibali na kusababisha vurugu.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: