Thursday, 19 April 2018

Esha Buheti amfunda mke wa Alikiba, “Wakikupa habari waambie mbona najua mume alishaniambia”

Msanii wa filamu Bongo, Esha Buheti amemfunda mke wa Alikiba, Aminah Khalef Ahmed wakati atakapo kuja Bongo na jinsi ya kuishi na watu wake.
Esha ambaye ni miongoni mwa watu wa karibu wa Kiba ambao wamesafiri mpaka mjini Mombasa kuhudhuria ndoa hiyo, ametumia mtandao wake wa Instagram kumfunda malkia huyo mpya wa Kariakoo.
Kupitia mtandao huo Esha Buheti ameandika:
ALHAMDULILLAH NDOA ISHAPITAA TUKUTANE KWENYE HALL USIKUU….. MASHALLAH MASHALLAH WIFI KARIBU NYUMBANI… UNAPOINGIAA KICHWA INAMISHA CHINI…MASKIOO WEKA PAMBAA…….WAKIKUPA HABARI WAAMBIE MBONA NAJUAA MUME ALISHANAMBIAAAA…..😆😆😆😆
Alikiba amefunga ndoa hiyo alfajiri ya leo April 19 katika msikiti wa Ummu Kulthummjini uliopo mjini Mombasa, Kenya.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: