Monday, 30 April 2018

Erasto Nyoni: Walinisahau nikawafunga


Mfungaji pekee kwenye mchezo wa watani wa jadi Simba SC dhidi ya Yanga SC, Erasto Nyoni amesema kuwa wapinzani wao walikuwa bize na washambuliaji, Emmanuel Okwi, John Bocco na winga Shiza Ramadhani Kichuya na hivyo wakajisahau kuhusu yeye ikawa ndiyo nafasi yake ya kupata goli hilo.

Kwenye mchezo huo uliyofanyika uwanja wa Taifa mwenyeji Simba ilipata bao lake kupitia kwa beki wake, Erasto Nyoni dakika ya 37 bao lililodumu mpaka dakika 90.

Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu tumeanza salama na tumemaliza salama, tunamuomba mungu tuweze kupata pointi tatu kutoka kwenye kila mechi.

Wao waliweza kujisahau wakajua wafungaji wetu ni Okwi, Bocco na Kichuya waliweza kunisahau mimi na nikaweza kufunga goli, sisi huwa tunajipanga kila mechi nadhani mwalimu ameweza kuona mapungufu yetu na atachukua hatua.

No comments:

Post a Comment