Edo Kumwembe auponda Uwanja wa Sabasaba

 Mwandishi na Mchambuzi wa Soka, Edo Kumwembe, ametoa maoni yake kuhusiana na ubovu wa Uwanja wa Sabasaba ambao una kibarua hivi sasa kati ya Njombe Mji FC dhidi ya Simba SC.

Edo ameeleza kuwa Uwanja huo hauna ubora wa kuridhisha kwa kusema kuwa haustahili kupewa hadhi ya kuchezea mechi za ligi.

"Simuoni Okwi. Well Watanzania tusiwe wajinga...tuna ushabiki wa kijinga sana wa Mpira...tuwageukie wanaotuongoza... Huu uwanja hauwezi kuwa wa Ligi kuu... Pitch bovu na halitoi matokeo halali...mchezaji Kama Okwi hawezi kudrible hata hatua sita...Mechi inazungumzwa saaana katika media lakini ukienda uwanjani ni upuuzi tu... Nakerwa na pitch mbovu.. Hazitupi hadhi za mechi ya Ligi kuu" ameandika Edo kupitia Facebook.

Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: