Wednesday, 25 April 2018

Dodoma yapiga marufuku nyama ya nguruwe

WAKATI leo mkoa wa Dodoma ukiwa mwenyeji wa maadhimisho ya sikuku ya Muungano halmashauri ya manispaa ya Dodoma imepiga marufuku biashara ya nyama ya nguruwe pamoja na mazao yake kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa homa ya nguruwe.

Kwamijibu wa taarifa iliyotolewa na Daktari wa mifugo manispaa ya Dodoma Dk, Innocent Kimweri jana alisema kuwa kwa mamalaka aliyopewa na kifungu namba 17 cha sheria ya magonjwa ya mifugo namba 17 ya mwaka 2003 anatangaza kuwa hivi sasa manispaa ya Dodoma inamlipuko wa homa ya nguruwe.

Alisema kutokana na hali hiyo kuanzia sasa anaweka zuio la biashara ya nguruwe pamoja na mazao yake hadi hapo itakapo tangazwa vinginevyo.

“Hakuna mnyama yeyote wa jamii ya Nguruwe, ngiri nguruwe pori au nguruwe wa kufungwa atakaye ruhusiwa kuingia au kutoka nje ya wilaya ya Dodoma pasipo ruhusa ya maandishi kutoka kwa daktari wa mifugo wa wilaya ya Dodoma mjini”alisema Dk, Kimweri

Vilevile alisema kuwa hakuna bidhaa inayotokana na nguruwe ikiwemo mbole, kinyesi, mkojo na damu kitakacho ruhusiwa kuingia au kutoka bila ya ruhusa ya maandishi kutoka kwa daktari wa mifugo wilaya.

Aidha alisema kuwa hakuna mnyama wa jamii hiyo atakaye kusanywa kwajili ya biashara pasipo ruhusa ya Daktari wa mifugo.

Kwa upandewake afisa habari wa manispaa ya Dodoma Ramdhani Juma, alipoulizwa juu ya taarifa hiyo alikiri kuwepo kwa ugonjwa huo wa mlipuko wa homa ya nguruwe na kuwataka wakazi pamoja na wageni kuchukua tahadhari

No comments:

Post a comment