Baadhi ya wanafunzi waliokuwa katika ukumbi wa mdahalo.
Mmoja wa wanafunzi washiriki katika mdahalo wa kuwapima kiuelewa  akizungumza.
Sehemu ya viongozi waliokuwa meza kuu.
Mkurugenzi wa shule za Feza, Ibrahim Yunus (kulia) akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi ma Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akimtunuku mwanafunzi aliyeshinda katika mdahalo uliohusisha shule za sekondari nchini na za nje.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi ma Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo, akiendelea kuwatunuku medali za ushindi.
Zoezi likiendelea la kutunuku medali.

WANAFUNZI mbalimbali kutoka Shule za Sekondari za serikali na shule binafsi hapa nchini wamepambanishwa na wanafunzi wengine kutoka nchi nane ikiwemo Kenya na Zimbabwe katika mdahalo wa kuwapima kiuelewa  kimasomo ambapo washindi walitunukiwa medali  za ushindi baada ya kufanya vizuri katika mdahalo huo.

Katika hafla ya kukabidhi vyeti iliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Kimataifa ya Feza, Salasala jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa shule za Feza, Ibrahim Yunus alisema mashindano hayo ya kimasomo yajulikanayo kama Africa Open Schools Debate Championships, yaliandaliwa na shule za Feza kwa kushirikiana na TAMISEMI.

Akizungumza katika hafla hiyo Yunus alisema kuwa lengo kubwa la midahalo hiyo ni kuwaandaa wanafunzi ili watakapomaliza masomo yao wawe na taaluma ya uelewa.  Mashindano hayo hufanyika kila mwaka, huu ukiwa mwaka wa pili kufanyika.

Alisema kuwa wanafunzi wa hapa nchini wameshiriki kutoka shule za serikali na binafsi  na nchi nane kutoka nje, ambapo miongoni mwake ni Kenya na Zimbabwe.


Kwa uapnde wake,  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi ma Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo alisema kuwa midahalo hiyo huwawezesha wanafunzi kuelewa masuala mbalimbali ya masomo na kuwapa mbinu za kujiamini mbele za watu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: