DK. SEMAKAFU AFANYA MAZUNGUMZO NA KAMPUNI YA KICHINA ITAKAYOSIMAMIA UJENZI WA VETA, MKOANI KAGERA


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  Dk. Ave Maria Semakafu amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Kampuni ya Ujenzi ya Kichina (CHINA QIYUAN ENGINEERING CORPORATION) ambayo inatarajia kusimamia ujenzi wa  Chuo cha Ufundi Stadi, VETA cha Mkoa wa KAGERA. 

Mazungumzo hayo yamefanyika leo katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo UDOM mkoani Dodoma ambapo kwa pamoja wamejadiliana hatua za awali za Ujenzi wa chuo hicho na kuwa tayari kampuni hiyo imekwisha andaa michoro ya namna chuo hicho kitakavyokuwa huku wakisisitiza kuwa ujenzi huo utafanyika kwa awamu mbili.

Kwa mujibu wa Meneja Mkuu Msaidizi wa kamapuni hiyo Fang Kefang amemweleza Dk. Semakafu kuwa awamu ya kwanza ya ujenzi huo itachukua miezi 18 na majengo yatakayojengwa yatakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi mia nne (400).

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano serikalini
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
3/4/2018

Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: