DIWANI WA SONGWA NGOLOMOLE AVUNJIKA BEGA AJALI YA NOAH KISHAPU


Diwani wa kata ya Songwa wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga Abdul Ngolomole (CCM)amevunjika bega la mkono wa kushoto baada ya gari aina ya Noah yenye namba za usajili T.219 CHT aliyokuwa anasafiria kuacha njia na kupinduka. 

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo Jumatano Aprili 4,2018, Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule amesema ajali hiyo imetokea jana saa 9 alasiri katika eneo la Mwangungulwa,kata ya Kolandoto kuelekea Kishapu. 

Amesema gari hilo likiendeshwa na Phabian Njile mkazi wa Maganzo –Kishapu liliacha njia na kupinduka na kujeruhi watu watatu akiwemo Abdul Ngolomole (28) ambaye alivunjika bega la mkono wa kushoto. 

Aliwataja wengine kuwa ni Abdallah Omary (32) mkazi wa Maganzo ambaye amevunjika paja la mguu wa kulia na Tayaya Masoud Rashid (29) mkazi wa Maganzo aliyepata madhara katika kiuno na mbavu. 

“Chanzo cha ajali ni mwendokasi wa gari husika na tunaendelea kumtafuta dereva ambaye alikimbia baada ya kutokea ajali hiyo na majeruhi wote wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyang,ameeleza Kamanda Haule. 

Na Kadama Malunde –
Muonekano wa Noah baada ya ajali
Muonekano wa gari baada ya ajali

Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: