Sunday, 15 April 2018

Diwani Ashambuliwa kwa mapanga

Jeshi la Polisi wilayani Tarime katika Mkoa wa Mara linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kumvamia kisha kumshambulia kwa bapa za panga Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji, pia Diwani wa Kata ya Sabasaba Khamis Nyanswi.

Kamanda wa Kanda Mkoa wa Kipolisi Tarime /Rorya Henry Mwibambe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na alisema kuwa, tayari watuhumiwa wote waliohusika  wamekamatwa na na wanaendelea na uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo.

"Alivamiwa akiwa njiani akimsindikiza mgeni wake kwenda kwenye usafiri huku akiwa anamchukua mgeni mwingine kumpeleka nyumbani Aprili 14, Mwaka huu Majira saa 3 usiku Mwenyekiti huyo alishambuliwa na kundi la watu hao kwa kumpiga bapa za panga  sehemu mbalimbali za mwili wake," alisema Kamanda.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Tarime, Lucas Ngoto alisema kuwa baada ya tukio hilo alipewa taarifa na kuthibitika kundi la watu watatu  lilimvamia na kuanza kumpiga kwa paba za panga na mawe lakini alifanikiwa kuwadhibiti japo alijeruhika.

Kaimu Mkurugenzi wa Kituo Afya DF  Sia  Bonifase alisema kuwa walimpokea Mwenyekiti huyo akiwa hajitambui Majira ya Saa 5 Usiku baada ya kupata matibabu maendeleo yake kwa sasa yako vizuri.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: