Madhimisho ya Sikukuu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo Tarehe 26/04/2018 Katika Wilaya ya Monduli yaliadhimishwa kwa kufanya usafi katika maeneo mbalimbali.

Zoezi hilo la kufanya usafi liliongozwa na Mh.Idd Hassan Kimanta ambalo aliongoza maelfu ya Wananchi na Wanafunzi Elimu ya juu na sekondari katika kufanya usafi katika maeneo ya Polisi,Hospitali ya Wilaya,sokoni na maeneo mbalimbali ya Mji wa Monduli

Maeneo mengine yaliyofanyika usafi ni Mto wa Mbu ambapo Wananchi ns askari wa JKT-Makuyuni walishiriki kwa wingi na Meserani wananchi walijitokeza kwa wingi.

Mkuu wa wilaya ya Monduli alishiriki kuzindua Chanjo mpya ya kuzuia Saratani ya mlango wa kizazi zoezi hilo lilifanyika katika hospitali ya Wilaya ya monduli Watoto wenye Umri wa miaka 9-14 walifika kupata chanjo hiyo.Pia wa mama walifika kupata vipimo vya uchunguzi saratani hiyo

Hata hivyo Kimanta amewataka wazazi, walezi na jamii nzima kuhakikisha wasichana wenye umri wa miaka 14, wanakwenda kupata chanjo hiyo huku akiwataka viongozi wa kata zote kusimamia zoezi hili kwa ufasaha na kuhakikisha hakuna mtoto atakayekosa chanjo hiyo pamoja na kuwaonya watu watakaokwamisha zoezi hilo kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
.
chanjo hiyo hutolewa bure kabisa
Share To:

msumbanews

Post A Comment: