Wednesday, 11 April 2018

DC ATOA ONYO KWA WATUMISHI WA SERIKALI WATAKAOSHINDWA KUSHIRIKI MICHANGO YA MAENDELEO


MKUU wa wilaya ya Busega mkoani Simiyu, Tano Mwera (aliyesimama) akizungumza kwenye baraza la madiwani mkuu lililofanyika wilayani hapo.

MKUU wa wilaya ya Busega mkoani Simiyu, Tano Mwera ametoa onyo kali kwa watumishi wa serikali watakaoshindwa kutoa michango ya maendeleo kwenye sehemu wanazoishi kwa kisingizio cha utumishi wa serikali.

Akitoa agizo hilo kwenye baraza la madiwani mkuu huyo wa wilaya aliwataka madiwani wote kwenda kuwasambazia watumishi wote wa serikali walio katika kata zao kushiriki kikamilifu michango yote ya kijamii ili kuhakikisha wanafanikisha malengo waliyojiwekea kwenye kijiji au kitongoji hicho.

Alisema kuwa kumekuwa na tabia za kutokushiriki kwa watumishi wa serikali kwenye shughuli za maendeleo mahali ambapo wanaishi kwa kisingizio cha kuwa ni mwajiriwa wa serikali hivyo awezi kuchangia michango ya aina yeyote ile katika jamii kwa madai kuwa serikali inawakata fedha za michango hiyo.

Aliongeza kuwa watumishi wanatakiwa kutambua kuwa nao ni wanajamii kama walivyo wengine hivyo wanatakiwa kutoa kila aina ya mchango unaokuwepo katika jamii wanazokaa kwa lengo la kusaidia maendeleo yanayopangwa na jamii ili kufanikisha kile wanachokihitaji kifanyike kwa maendeleo ya yote hivyo mnatakiwa kuchanga kama wanavyofanya wengine.

“Kwa mtumishi ambaye atakiuka agizo la uchangiaji wa maendeleo katika wilaya yangu basi jera inamuhita kwa kugoma kuchangia”

Kwa upande wake diwani wa kata ya Imalamate Richard Magoti amempongeza mkuu wa wilaya hiyo kwa kutoa tamko hilo kwani ilikuwa ni changamoto iliyokuwa ikiwasumbua juu ya majibu waliyokuwa wakiyapata kutoka kwa watumishi wa umma katika suala la michango ya maendeleo.

Aliongeza kuwa katika kata yake changamoto hizo zilikuwa zinajitokeza lakini kulingana na uelewa wa baadhi ya watumishi walikuwa wakishiriki katika zoezi la uchangaji wa fedha katika kufanikisha miradi ya maendeleo inayokuwa na ubunifu kutoka kwa wananchi ili iweze kuwasaidia kwenye vijiji vyao.


Aidha Magoti amemtaka mkuu huyo wa wilaya kulisimamia kikamilifu jambo hilo kwani watumishi wengi wa serikali wamekuwa sio miongoni mwa jamii kutokana na kutokushiriki kikamilifu katika ufanikishaji wa miradi katika jamii.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: