Katibu Tawala wilaya ya Arumeru, Timoth Mzava amewaagiza wananchi wa kata za Kiranyi na Oloirien halmashauri ya Arusha, waliojenga uzio wa kuta kwenye nyumba zao zinazozuia maji kupita, kubomoa mara moja ili kuruhusu maji kupita wakati wa mvua ili kuepusha madhara makubwa zaidi yanayoweza kutokea.    
Katibu Tawala huyo, ametoa agizo hilo kufuatia madhara waliyoyapata wakazi wa kata hizo, yaliyotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha, karibu maeneo yote Tanzania na kuwasababishia hasara kubwa wakazi hao.    
Hata hivyo Mzava amefikia uamuzi huo mara baada ya wananchi hao wenyewe, kumuelezea sababu za maji hayo ya mvua kuharibu mali zao, wakati alipowatembelea na kujionea madhara waliyoyapata ikiwemo kuta kuanguka na maji kujaa ndani ya nyumba zao, na kusababisha uharibifu wa thamani zote za ndani  huku wengine wakilazimika kuhama nyumba zao kwa hofu.     
Wananchi hao, wamemueleza Katibu Tawala kuwa, maji yanajaa na kuingia kwenye nyumba za watu, kutokana na ubinafsi wa kila mtu kujijengea kuta kuzunguka mipaka ya kiwanja na kusababisha maji kukosa mwelekeo na kuleta madhara hayo yaliyotokea.      
Titus Mrema mkazi wa Kirayi amesema kuwa, pindi mvua kubwa zinaponyesha, maji hukosa mahali pa kupita kutokana na kuta zilizojengwa na badala yake hujaa ndani ya nyumba za watu na kusababisha madha haya mnayoyaona.     
Wananchi hao walimtembeza katibu Tawala na kushuhudia namna uzio wa kuta zilivyojengwa na kuzuia maji kupita,  jambo lililosababisha baadhi ya kuta kuanguka na nyingine kutobolewa kwa dharura ili kuruhusu maji kupita.    
Baadhi ya wananchi wamesema kuwa chanzo cha maji hayo kukosa uelekeo ni kubomolewa kwa tuta lilolopo katika eneo la Kiyoga, lililokuwa limejengwa na wazee miaka ya nyuma, kwa lengo la kupunguza kasi ya maji na maji hayo kuelekezwa mtoni.
Samwel Ngarabali mkazi wa Ilkiding'a na diwani mstaafu amemthibitishia Katibu Tawala kuwa, jambo la msingi ni kudhibiti maji eneo la Kiyoga na Olturoto,ambapo hapo awali kulikuwa na tuta linalozuia maji na kuelekeza maji hayo mtoni, lakini kuna watu wamebomoa tuta hilo kuepusha maji kupita kwenye mashamba yao, jambo linalosababisha madhara kwa wakazi waishio maeneo mengi ya kanda za chini.      
Hata hivyo Mzava ameunda timu ya watalamu kuchunguza zaidi  na kuthibitisha ukweli juu ya tuta hilo, eneo la Kiyoga na kutafuta namna ya kudhibiti maji hayo katika eneo hilo.     
Naye Hussein Hudison, mkazi wa Ilkiurei ameunga mkono agizo hilo la Katibu Tawala, na kusema kuwa inawabidi wakakae mkutano wa kitongoji na kukubaliana kwenda kubomoa kuta hizo kwani watu wote wanafahamika, na kukaa na kukubaliana na watu hao ikishindikana, wananchi kwa pamoja kuamua kufanya maamuzi magumu.      
Hussein Hudison mkazi wa Ilkiurei ameunga mkono agizo hilo na kusema kuwa inawabidi wakakae mkutano wa kitongoji na kukubaliana kwenda kubomoa kuta ambazo zinasabanpbisha madhara hayo, kwani watu wote waliojenga kuta zinazozuia maji zinafahamika, na kukaa na kukubaliana na watu hao ikishindikana, wananchi kwa pamoja kuamua kufanya maamuzi magumu.     
Mpaka inaandikwa habari hii, bado haijafahamika thamani halisi ya hasara ya mali za wananchi iliyopatikana kutokana na mvua hizo, thamani halisi itatolewa baada ya watalamu kukamilisha tathmini hiyo.

Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha  Application yetu ya Msumba News ili upate habari zetu kwa wepesi zaidi kama vile Magazeti kuliko ilivyo sasa.


Tumekurahisishia; 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: