Saturday, 14 April 2018

CHELSEA YAFUFUKA KWA KUTOA KIPIGO CHA 3-2 DHIDI YA SOUTHAMPTON
Kikosi cha Chelsea kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 ugenini dhidi ya Southampton FC katika mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa mchana huu.

Southampton waliokuwa nyumbani walianza kucheka na nyavu kupitia Tadic kwenye dakika ya 21, kisha Bednarek akifunga pia dakika ya 60.

Chelsea walirejea kwa nguvu kuanzia dakika ya sabini kwa kuliwinda lango la Southampton ambapo katika dakika ya 70, Olivier Giroud alitupia kambani huku Harazd akifunga la pili kwenye dakika ya 75.

Giroud aliingia kambani tena kwa mara ya pili kwenye dakika ya 78 kwa kuipa bao la ushindi Chelsea na mchezo ukimalizika kwa mabao 3-2.

Ushindi unaifanya Chelsea kufikisha alama 60 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: