BREAKING: MBOWE NA WENZAKE WATIMIZA MASHARTI, MDEE AUANGISHWA


Viongozi wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wao, Freeman Mbowe wametimiza masharti ya dhamana katika kesi yao Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Machi 3, 2018. Mahakama hiyo imejiridhisha na nyaraka zilizowasilishwa mahakamani.

Masharti ya dhamana yalikuwa ni kila mshtakiwa kuwa wadhamini wawili watakaosaini bondi ya TZS 20m, barua ya utambulisho toka serikali za mtaa.

Aidha, Mbunge wa Kawe, Halima Mdeeamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar ili kusomewa mashtaka yanayomkabiri.
Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi ameomba kufanya marekebisho ya hati ya mashtaka ili kumjumuisha Mdee katika kesi inayowakabili viongozi wenzake sita wa Chadema wanaokabiriwa na mashataka manane yakiwemo ya uchochezi, uasi na kuhamasihsa maandamano. Hata hivyo Mahakama imempa dhamana baada ya kuridhika na Sifa za Wadhamini.

Mbowe na wenzake ambao ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji na manaibu wake wa Bara na Zanzi­bar, John Mnyika na Salum Mwalimu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wote wanakabiliwa na mashtaka manane yakiwemo mawili ya uchochezi wa uasi yanayom­kabili Mbowe na wanatarajiwa kuachiwa kwa dhamana leo.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: